MAMBO
MATANO MUHIMU KATIKA KUIMARISHA MAHUSIANO
Mahusiano ni nguzo muhimu
sana katika maendeleo ya jamii yoyote hasa yanapokuwa ni mahusiano chanya.
Binadamu ni mnyama wa kijamii (social animal) ambaye mafanikio yake
yamejiegemeza moja kwa moja kwenye ushirikiano ambao ni zao la mahusiano
chanya.
Fikiria maisha yangekuwa
na sura gani ikiwa kila binadamu angekuwa anaishi kipweke pweke?
Kuna aina mbalimbali za
uhusiano, miongoni mwa hizo ni urafiki, mapenzi, uhusiano wa kifamilia,
uhusiano wa kikazi nk.
Mambo ya msingi katika
kudumisha uhusiano wa aina yoyote ni pamoja na:-
1. MAWASILIANO
Mawasiliano ni miongoni
mwa mambo yanayoashiria kujali na hivyo kuleta ustawi katika mahusino ya aina
yoyote. Mtu anapowasiliana nawe kupitia namna yoyote ile haina shaka kwamba
anakukumbuka, anakuthamini na anakujali.
2. UAMINIFU
Ili mahusiano yoyote
yaweze kudumu uaminifu ni nguzo muhimu sana. Uaminifu katika matendo na ahadi
zinazotekelezeka tena kwa wakati ni kichocheo cha mauhusiano imara.
3. MSAMAHA
Imesikika mara nyingi
kwamba hakuna binadamu mkamilifu, kumbe ndiyo hicho kinachomfanya binadamu huyu
awe na mapungufu na hapa na pale. Hatahivyo kuna wakati tunahitaji kusameheana
lakini pia kuomba msamahama wa dhati kwa makosa tuliyoyafanya ili maisha yaendelee
katika ustawi ule ule.
4. MUDA
Ili mahusiano yoyote yawe
imara ni lazima watu watenge muda wa kukaa pamoja kujadili mambo yao,
kubadilishana uzoefu na kupeana mawazo mapya. Hii inajenga ukaribu na
ushirikiano.
5. TABASAMU
Tabasamu katika mahusiano
ya aina yoyote maranyingi huonyesha hisia chanya miongoni mwa watu na hivyo
kuufanya uhusiano usiwe na mashaka.
Fikiria unamchangamkia
rafiki yako, mpenzi wako au mzazi wako kwa furaha na bashasha halafu ndio
kwanza yeye haonyeshi kujali, utajisikiaje?
By Kato
Ans. (Editor in chief)
No comments:
Post a Comment