DAWA RAHISI YA VIDONDA VYA TUMBO UNAYOWEZA KUTENGENEZA MWENYEWE.
Vidonda
vya tumbo ni majeraha ndani ya tumbo ambayo hutokea wakati ute unaolinda utumbo
unapokuwa umeharibiwa.
Tafiti zinaonyesha kuwa, angalau mtu mmoja kati ya watu kumi
anasumbuliwa na vidonda vya tumbo.
Tafiti zinaonyesha kuwa, angalau mtu mmoja kati ya watu kumi anasumbuliwa na vidonda vya tumbo.
NINI HUSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO?
Miongoni mwa vitu vinavyosababisha vidonda vya tumbo ni matumizi
ya mara kwa mara ya madawa (Non-Steroidal Anti Inflammantory Drugs) kama
Diclofenac, Aspirin, Meloxicam nk. Dawa hizi huchangia kuharibika kwa ute
unaolinda utumbo na kuufanya utumbo uweze kushambuliwa na asidi za tumboni kwa
urahisi na hivyo kusababisha vidonda vya tumbo.
Vile vile tafiti mbalimbali zinataja matumizi ya
vilevi/pombe na sigara kuchochea vidonda vya tumbo. Walevi na wavuta sigara
wanatajwa kuwa katika hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo kuliko wasio
tumia. Lakini pia msongo wa mawazo ingawa hausababishi moja kwa moja vidonda
vya tumbo ila hufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa ambao tayari ni wagonjwa.
Miongoni mwa dalili za mtu kuwa vidonda vya tumbo ni kukosa
hamu ya kula, kichefuchefu,kizunguzungu, uchovu wa mara kwa mara bila sababu ya
msingi, kukosa usingizi, maumivu ya kifua, tumbo kujaa gesi n.k.
DAWA RAHISI YA VIDONDA VYA TUMBO
- CHUKUA PAPAI BICHI KABISA NA ULIOSHE VIZURI.
- USILIMENYE WALA KUONDOA MBEGU ZAKE.
- BAADA YA KULIOSHA KIKAMILIFU, BILA KULIMENYA LIKATE KATE VIPANDE VDOGO VIDOGO MITHILI YA HIVI HAPA CHINI.
- WEKA VIPANDE HIVYO KWENYE CHOMBO SAFI, KWA MFANO JAGI.
- WEKA MAJI SAFI HADI USAWA WA VIPANDE HIVYO ULIVYOKWISHA WEKA KWENYE CHOMBO CHAKO.
- TUNZA MCHANGANYIKO HUO (VIPANDE VYA PAPAI VIKIWA VIMELOWEKWA KWENYE MAJI) KWA SIKU NNE. HESABU SIKU, KWA MFANO KAMA UMELOWEKA MCHANGANYIKO HUU JUMATATU, ANZA KUHESABU JUMANNE, JUMATANO, ALHAMISI NA IJUMAA ITAKUWA SIKU YA NNE.
- SIKU HIYO YA NNE, MAJI YATAKUWA YAMEBADILIKA RANGI NA KUWA MEUPE, CHUJA VIZURI KUTENGANISHA MAJI NA VIPANDE VYA PAPAI NA KIMSINGI MAJI HAYA NDIO TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO.
DOZI
KUNYWA NUSU GLASI YA MAJI HAYA KILA SIKU ASUBUHI, MCHANA NA
JIONI. HAUTASIKIA TENA MAUMIVU KWASABABU MAJI HAYA YANATIBU KABISA VIDONDA VYA
TUMBO AMBAVYO VINAKUSABABISHIA MAUMIVU UNAYOYASIKIA. UTAENDELEA KUNYWA KWA
UTARATIBU HUO KWA WIKI KADHAA, HII INATEGEMEA UMEISHAATHIRIKA KWA KIASI GANI NA
VIDONDA HIVI, HIVYO TUMIA DAWA HII HADI UTAKAPOPONA KABISA. HATA HIVYO NI MUHIMU
KUPIMA ILI KUJUA KIASI CHA MAENDELEO UTACHOKUWA UMEFIKIA (RECOVERY).
DAWA HII SIYO KWA AJILI YA KUTULIZA MAUMIVU BALI
NI TIBA KAMILI YA VIDONDA VYA TUMBO.
No comments:
Post a Comment